Skip to main content

Sababu 6 Kwa nini Biashara Yako Inahitaji Tovuti.

1. Kupata uaminifu mkubwa wa biashara kutoka kwa wateja
Kutokana na kuwepo kwa matumizi makubwa ya intaneti asilimia kubwa ya watu wanaperuzi mtandaoni kutafuta bidhaa mbalimbali zinakopatikana. Kwa kumiliki tovuti, biashara yako itakuwa kwa kasi na kuaminika zaidi. Biashara isiyokua na tovuti hupelekea wateja kukosa Imani nayo, hivyo wanunuzi kwenda kununua kwenye biashara inayoaminika yenye tovuti. Ikiwa tayari biashara yako ina tovuti isiyokidhi viwango, ni vyema kufanya/kutengeneza upya kwa utaalamu wa hali ya juu ambayo itahamasisha biashara kukuwa na kuaminika. Pia biashara ambazo zinafanyika majumbani inasaidia sana kukuza na kufanya biashara ijulikane ulimwenguni kwakua haihitaji kuwa na ofisi maaluma kwa ajili ya bidhaa zako.


2. Gharama za kumiliki tovuti ni rahisi sana
Kama mmiliki wa biashara labda unafikiri huwezi kumudu tovuti ya kitaalamu, lakini ni vigumu kuendesha biashara bila kuwa na tovuti. Ingawa gharama ya kutengeneza tovuti inatofautiana inapokwisha, tovuti ya biashara ina gharamu kiasi cha chini ya dola 400, wakati mwingine, ni dola 250 tu. Ikilinganishwa na ghrarama za matangazo ya magazeti, unapofikiria upatikanaji wa soko kwa kupitia tovuti ni mkubwa zaidi kulinganisha na hizi njia nyingine.


3. Inawezesha kufatilia wateja wako kirahisi
Hii ni njia rahisi na bora ya kusahisha taarifa kuhusu huduma na bidhaa kwenye tovuti yako kuliko kutumia nyaraka za kuchapisha kama magazeti,vipeperushi,au majarida. Pia tovuti ni njia bora ya kuwawezesha wateja wako kufahamu bidhaa mpya zilizowasili kwenye biashara, vilevile katambua matukio yajayo, matangazo maalum, au huduma zingine zingine unazotoa. Tofauti na matangazo ya kuchapisha ambayo baada ya kusomwa tu huwezi kuongeza habari au kupuguza, tovuti yako inaweza kutoa taarifa zilizopo kwenye biashara na ikawafikia watu wengi zaidi.


4. Hupatikana kila mahali na kwa muda wowote
Tovuti hupatikana kwa wateja wako wote wa kawaida na wenye uwezo 24/7/365 kuwapa urahisi wa kuchunguza na kuchagua bidhaa na huduma zako wakati duka au ofisi imefungwa. Kwa maisha ya leo, hii ni hatua kuu mteja anayoifanya kabla ya kuchukua uamuzi wa kununua.


5. Tovuti ya kulenga soko kubwa
Ikiwa unatoa bidhaa au huduma, tovuti yako itatoa sehemu mbadala ya kuuza. Kama muuzaji, tovuti ina nafasi nzuri ya kuuza bidhaa zako kwenye soko pana na kubwa, pia huduma zinaweza kupatikana duniani kote. Je haudhani kama utaweza kuuza bidhaa zako au huduma zako mtandaoni? Usisahau, hata magari na nyumba zinauzika mtandaoni!


6. Tovuti inakupa nafasi ya kuonyesha kazi/bidhaa zako kwa watu
Bila kujali aina gani ya biashara unayofanya, tovuti ni mahali pazuri pa kuonyesha kazi yako. Kwa kuweka picha ya kazi ulizokwishafanya au unazozifanya, pamoja na ushuhuda kuhusu kazi yako, unaweza kuonyesha nini kinachofanya biashara yako kuwa ya kipekee ukilinganisha na zingine.

 

Bonyeza hapa kuwasiliana nasi ili upate Website Bora